The Serengeti Awards Take Place this 31 January 2026

Mount Meru Hotel — Check Your Invitation

WAZIRI KIJAJI AKAGUA MAANDALIZI YA TUZO ZA “THE SERENGETI AWARDS” 2025

Sixmund Begashe, Arusha

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ameridhishwa na maandalizi ya hafla ya tuzo za The Serengeti Awards, na kuipongeza timu nzima ya maandalizi kwa kazi kubwa iliyofanya.

Dkt. Kijaji akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt.Hassan Abbasi, Naibu Katibu anayeshughulikia Utalii Bw. Nkoba Mabula na Menejimenti ya Wizara pamoja na viongozi wa Taasisi zake, amefanya ukaguzi wa maandalizi ya tuzo hizo kubwa nchini zinazotarajiwa kufanyika leo tarehe 31 Januari 2026 huku Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba.